|
Naendelea na kufafanua tatizo la watangazaji wetu katika Lugha.Mimi huwa nashangaa wanapopata tabu kusoma salamu za wasikilizaji wao pale wanaposema "salamu kwa Mume wangu......'au "salamu kwa Mke wangu......".Wao lazima wabadili kwa kuweka Mume wake au Mke wake.Wanaona ni matusi kusoma kama ilivyoandikwa ilhali katika Qur'an Allah (S.W) amesema kutwambia viumbe vyake kama ifuatavyo: وَقَالَ رَبُّكُمُ ادْعُونِي أَسْتَجِبْ لَكُمْ إِنَّ الَّذِينَ يَسْتَكْبِرُونَ عَنْ عِبَادَتِي سَيَدْخُلُونَ جَهَنَّمَ دَاخِرِينَ Na Mola wenu Mlezi anasema: Niombeni nitakuitikieni. Kwa hakika wale ambao wanajivuna na kuniabudu Mimi wataingia Jahannamu wadhalilike. (Qur.40:60). Hapo penye kijani tunaposoma huwa hatuna maana kuwa sisi ndio tunaojibu.Kila anayesikiliza anajuwa kwamba tunamkusudia Allah s.w pekee kuwa ndiye anayejibu dua zetu,viumbe wake.Huo ni mmoja tu ya mifano kutoka katika Qur'an. Katika ufahamu wa lugha ni kawaida anayesikiliza kuhamisha mawazo yake na kujiona kama kwamba anamsikiliza mtu wa tatu aliye mbali badala kukusikiliza wewe unayesema.Inapokuwa hamjui huyo mtu wa tatu basi huunda picha ya mtu na mazingira tofauti na anayetangaza.Hapo huwa ndipo inapotimia ladha ya usikilizaji kwani anayesikiliza huhama kimawazo na kujikuta yuko sehemu nyengine tofauti na alipo. Hivyo kunakili maneno ya mtu mwengine ni moja ya vivutio vya lugha na wala si matusi au kosa, na ndio upana wa lugha. |