Kikwete kuzipatia ufumbuzi kero za maji na ardhi  Muheza

Kikwete kuzipatia ufumbuzi kero za maji na ardhi Muheza

Na Salim Mohammed  Muheza. Ijumaa 28/03/2014   Rais Jakaya Mrisho Kikwete amewaambia wakaazi wa Wilaya ya Muheza Mkoani Tanga kuwa matatizo yao ya  uhaba wa ardhi kwa ajili ya kilimo na makazi Wilayani humo yatalimaliza kabla ya kwisha kwa kipindi chake cha Urais    Akizungumza kati...

Viongozi wa waislamu waaswa kuchunga umoja wao

Viongozi wa waislamu waaswa kuchunga umoja wao

      Karibu Istiqaama-Tanga Islamic Secondary School.Contact:+255773476609 VIONGOZI WA WAISLAMU WAASWA KUCHUNGA UMOJA WAO  Jumanne 10 Dhulhijja 1434H,15/10/2013    Wanazuoni wa kiislamu kwa mara nyenngine tena wamehimizwa kurejesha umoja wao ili kuulinda uislamu dhidi  ya maadui wa...

Udhaifu wa waislamu unatokana na dhulma –Sheikh

Udhaifu wa waislamu unatokana na dhulma –Sheikh

  Alkhamis,1 Shawwaal 1434H,8/08/2013 Sheikh Salim Bafadhil,naibu mudiir wa Ansaar Sunna amebainisha vyanzo vinavyopelekea udhaifu mkubwa unaowakumba waislamu wa enzi hizi. Ubainifu huo umebainika   katika  khutba  aliyoitoa mara baada ya swala ya Idul Fitr iliyoswaliwa kwenye viwanja vya Ta...

Maimamu Tanga waichambua rasimu ya katiba

Maimamu Tanga waichambua rasimu ya katiba

Jumatatu 29Shaaban 1434 H;8/07/2013. Maimamu wa misikiti mbali mbali ya jijini Tanga wamekutana kwenye ukumbi wa Simba Mtoto katikati ya jiji hilo kwa madhumuni ya kuangalia makosa yaliyomo kwenye rasimu ya katiba mpya na kutoa mapendekezo yao yatakayopelekwa kwenye baraza la katiba la kiislamu lita...

Current Southern Moon Phase

RAMADHANI 1435H

RAMADHAAN 1435H
KUJUA TAREHE YA LEO BOFYA KALENDA HAPO JUU,BOFYA TENA KUKUZA HALAFU  ANGALIA.

ASILI YA UONGOFU JUZUU YA 1ASILI YA UONGOFU JZ2ASILI YA UONGOFU JZ4ASILI YA UONGOFU JZ11ASILI YA UONGOFU SASA IMEKAMILIKA .PATA JUZUU ZOTE 18 KWA BEI NAFUU.

مركز النور الاجتماعي في دبلن - ايرلندا

            Madrasat Noor-Ireland

Kura za maoni

Unaionaje dola ya kiislamu ya ISIS makao makuu Iraq
 

Na Philip Rawson, Mfasiri Abu Kawthar

 Kazi kubwa ya awali ya usanifu majengo wa Kiislamu ilifanyika katika kipindi cha maisha ya Mtume, swallallahu alayhi wa sallam. Huu ulikuwa ni ujenzi mpya wa Ka’ba mjini Maka. Kazi hii ilifanywa na fundi seremala, yamkini, muhabeshi. Kuta zilipambwa kwa picha za kuchora za Maria, Yesu, Ibrahim, Manabii, Malaika na miti.

 Makatazo ya picha yalikuja katika karne ya nane, na yalikuwa katika Hadith, sio Qur’an. Aina kuu za usanifumajengo wa Kiislamu ni Msikiti, mnara, ngome na kasri. Mabafu ya kuogea, makulateni na usanifumajengo mdogo-mdogo ulifanyika kwa kuigizia usanifu huo mkubwa wa majengo.

 Kimsingi, Msikiti ni nyumba ya ibada, na ni kituo cha jamii ya Kiislamu. Wenyewe haukulazimu kuezekwa paa kama ilivyokuwa katika zama za nyuma na baadae India. Katika ukuta mmoja au zaidi kulikuwa na paa au kuba ambazo zilileta mvuto wa usanifumajengo, nao muundo wa minara ya Kiislamu ulikuwa na mvuto wake. Ndani ya Msikiti, kuna sehemu nne kuu; mihrabu, mimbari, pazia na marufaa ya kuwekea Qur’an, makulateni ya kutilia udhu.

 Mihrab ni pembe ya kuonesha uelekeo wa kibla (kuelekea Maka iliko Ka’ba).Kwanza kabisa, mihrab ilianzia Madina (707 A.D). Mara nyingi mihrab ilikuwa ikipambwa kwa tepe na milango ya mbao ya ukutani yenye mapambo.

 Mimbari ni kiriri kilichoinuka juu, mara nyingi, kikiwa kimezibwa kwa juu. Pazia ndiyo inayounda faragha kwa kuizunguushia mihrab. Marufaa au meza ya kuwekea Qur’an mara nyingi ilijengwa kwa mawe huku ikiwa na nguzo, na kulateni nalo huzibwa kwa juu. Misikiti mikubwa ya awali ilijengwa nchini Iraq, katika miji ya Basra na Kufa kwa kutumia maarifa ya ufundi ya wenyeji, kwani hiyo ilikuwa ni misikiti ya awali kabisa kutwaliwa katika nchi hizo.

  Misikiti hiyo iliezekwa paa, zikiwa na kuba zisizo na pau ambazo nguzo zake zilichukuliwa katika majengo ya zama za ujahili.Hata hivyo, ilikuwa ni Misri ambayo mnamo mwaka 673 AD iliongeza minara ya pembe nne katika jengo. Huenda waliiga minara ya pembe ya Hekalu la Temenoi la Syria ambalo liligeuzwa kuwa msikiti kama ilivyokuwa kwa Msikiti mkubwa wa Damascus, msikiti mkongwe wa Ijumaa uliosalia hadi leo.

  Sehemu nyingine (kwa mfano katika msikiti wa Qairawan), mnara mmoja mkubwa ulikuwa katikati ya viambaza viwili vya ndani.Mnara wa awali wa kumbukumbu ya usanifumajengo wa Kiislamu (ulioanza mwaka 643 AD) ambao ulikuwa ni kazi ya mafundi kutoka sehemu zote za Dola ya Kiislamu, ulikuwa ni Kuba ya Jabali kwenye msikiti wa Bait-ul-Muqaddas, unaoaminika kuwa ndipo mahali ambapo Mtume, swallallahu alayhi wa sallam, alianzia safari yake ya kwenda mbinguni.

 Ni wa muundo wa‘rotunda’ ulioigwa na makanisa ya Kikristo ndani ya Bait-ul-Muqaddas, ghorofa yenye muundo wa pembe nane, kuba la duara la ndani lililozunguuka Jabali likishikilia mihimili minne na nguzo 12, sehemu ya juu ya ukuta yenye madirisha 16, iliyowekwa kuba la mbao.Hiyo ni muhimu kwa ajili ya uwazi mkubwa wa sehemu zake, na kwa ajili ya uzuri wa mapambo yake.

  Awali sehemu ya nje kama ilivyokuwa ya ndani, ilifunikwa kwa mapambo ya picha. Miji mikuu ilipambwa kwa sanaa ya miti iliyotengenezwa kwa maandishi ya maua, kulikuwa na sanaa za urembo wa kuchonga na kutia marumaru.

 Kulikuwa na sanaa ya sahani za bati.Msikiti wa kwanza kabisa wa mawe, ule wa Damascus (ulioanza mwaka 707 AD) wenye mjengo wa pembe nne za mraba, ambao bado upo, ndio unaohifadhi masalia ya urembo bora wa ndani.

 Papo hapo pia kipo kielelezo cha nakshi bora za usanifumajengo wa Kiislamu, grili za dirisha la jiwe la kuchonga, lililowekwa kwenye jengo.Orodha ya Makasri ya jangwani ndiyo inayoweka msingi wa maendeleo zaidi.

 Jengo la Quasayr Amra (715 AD) ndilo jengo la kwanza kabisa la kisasa likiwa na pau na kuba ya mawe madogo-madogo ya kuchonga, likiwa na vikuku, katika mawe likiwa na urembo wa sanamu na kusakafiwa kwa urembo wa vioo. Hiyo ilikuwa ni aina ya kasri iliyorudiwa-rudiwa kwa namna mbalimbali nchini Syria.

 La kuvutia zaidi kati ya Makasri hayo ni Mschatta (karne ya 8). Hili lilikuwa na kuta za mraba za matofali, likiwa na minara ya pembe na minara mitano ya nusu mviringo kila upande. Jengo la ndani lilibakia katika hatua mbalimbali za mwisho. Sehemu yake ya kuvutia zaidi ikiwa ni tepe zake za kuburudisha zilizorembwa mno kwa urembo wa taswira.

 Chini ya Utawala wa Banu Abasi mjini Baghdad, vigezo vya kuvutia zaidi vya usanifu majengo wa baadae vikawekwa. Baghdadi yenyewe, kwa asili yake, ulikuwa ni mji uliopangika bila kuwepo maarifa ya utangulizi.

  Mnamo mwaka 762, maelfu ya mafundi walikusanywa na kazi ikaanza. Yasemekana plani ilichorwa kwa mistari ya majivu ardhini ili Khalifa Mansour aweze kuona vizuri.Plani lilikuwa ya duara, ikiwa na takribani mita 2,638 za mapana, malango manne yaliyopewa majina ya majimbo ambako yalifungukia.

 Kuta za matofali zilizoambatana na uzio uliosukwa kwa nyasi angalau ulimalizwa kujengwa ndani ya miaka minne. Kila lango likiwa na njia za kuingilia-lilikuwa na ukumbi wa hadhara juu yake ukiwa umeezekwa kuba iliyotonewa dhahabu.

 Isfahan nayo pia, kiasili, ilisemekana kujengeka kwa plani hiyo ya duara. Ikiwa na takribani mita 3,000. Katikati yake kulikuwa na kasri na msikiti mkubwa. Kasri likiwa na ukumbi wa kuba wenye njia za chini kwa chini na kuba tupu, lilijengwa kwa mawazo ya kujikweza, yamkini hivi ndivyo walivyopenda Banu Abasi, kuwa na makasri yenye kumbi za hadhara mara nyingi zikiwa na kuba, na safu za vyumba vya kuingia watu.

 Chini ya Banu Abbas, sura ya msikiti ilibadilika mno. Ile aina ya zamani isiyo na pau ndiyo ikatawala. Katika msikiti wa Raqqa na kwingineko, paa zilikuwa juu ya pau. Baadhi kama vile msikiti mkubwa wa Sammara (842 AD), nao kama ulivyo ule wa Raqqa, umewekwa minara inayofanana na ngome za mji huo. Samarra pia inafahamika kwa urembo wa taswira.

 Hatua muhimu ya maendeleo katika karne ya 8 na 9 enzi za Ukhalifa wa Banu Abbas, ilikuwa ni ile ya kubadili safu za kuba na pembe za kuta za mihrab. Msikiti wa Aqsa kule Bait-ul-Muqaddas (760 AD) ni mfano hai. Hiyo yaweza kuonekana katika pande za magharibi kupitia Misikiti ya Ibn Tulum (Cairo), Qairawan (Tunis) hadi Cordova.

 

HABARI ZA UAMSHO

   Wamefika lakini bado wanakwenda

Wasafiri kati ya  kisiwa cha Pemba na Tanga wakishuka Mashua katika bandari ambayo sio rasmi eneo la Sahare mjini Tanga kufuatia kutokuwa na meli kwa kipindi kirefu na hivyo kutumia usafiri huo pamoja na ngalawa  ambao ni hatarishi hasa vipindi vya upepo wa kusi.


   Jisajili au Rudi ukumbini ili kuweza kuchangia

 

 MWANGAZA KWA UMMA

  WAUMINI WA AKHERA NA VITU VYA DUNIA

 Na Abu Kawthar

Hamaniko la mwanadamu na tamaa yake kubwa ya kutaka vitu vya dunia imemzuzua kiasi cha kuona kama vile imani juu ya Maisha bora ya Akhera inamchelewesha na inaweza hata kumtia umasikini!

Watu wanaohaha  kuitafuta dunia ndio wanaoonekana wa maana zaidi machoni mwa waumini wa dunia. Ukiwa na nyumba au majumba na gari au magari, basi wewe ndio ‘mtu wa maana’ kwao katika dunia hii!

Vitu hivyo havitazamwi  kama ni mapambo ya dunia na nyenzo tu za kuitafutia Akhera, bali vinatazamwa kama lengo kuu la maisha! Ukionekana unatumia muda wako mwingi katika dini unaonekana kama “mwinyi” fulani tu. Lakini ukuonekana katika pilikapilika au mishemishe za kutafuta maisha ya dunia zisizojali hata muda wa ibada basi wewe ndio ‘mtu wa maendeleo’.

Dhana kuwa kutafuta dunia ndiyo maisha imewafanya baadhi ya watu wapuuze kabisa hata wajibu wao wa kumwabudia Mola wao. Wengine wamewatazama kwa jicho la dharau wale wanaohaha kuitafuta Akhera na kuwaona kama si watu wa maendeleo. Wanawakadiria mpaka maisha yao!

 

 

Videos

 

                                                                                  

                        SHEIKH ALLY BOHERO-WANAFIKI                                                   Furaha-Skh Othman Maalim                 Uharamu wa muziki.Sheikh Kishki